Wakazi Wa Nakuru Walalamikia Ukosefu Wa Usalama Katika Eneo La Makaburi La Nakuru

Wakazi wa Nakuru wamelalamika kuhusu ongezeko la visa vya utovu wa usalama katika eneo la makaburi la Nakuru Kaskazini ambako wapendwa wao wamezikwa. Wakazi hao wamesema eneo hilo la makaburi limegeuka kuwa makazi ya watoto wanao-randa randa mitaani ambao huwashambulia na kuwapora watu wanaozuru eneo hilo. Wakazi hao sasa wanahofia kuwa huenda eneo hilo la makaburi likawa hatari kwa binadamu. Ua unaozingira eneo hilo la makaburi pamoja na lango kuu vimebomolewa na watu wasiojulikana. .