Wakazi wa Mombasa waandamana kupinga mahali pa kutupia taka

Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho ameangaziwa kutokana na mrundiko wa taka taka katika kaunti hiyo. Wakazi waliandamana kupinga agizo la kutupa taka taka katika maeneo matatu pekee wakisema hatua hiyo itasababisha kuzuka kwa maradhi. Wakazi hao waliosema hayo katika eneo la kutupa taka la Liwatuni, walilalamika kuwa hatua ya kutenga majaa ya Kibarani, Mwakirunge na Shonda kuwa maeneo ya kutupa taka taka itawanyima ajira. Pia wamehofia kuenea kwa maradhi kutokana na mazingira machafu. Walilaumu serikali ya kaunti hiyo kwa kushindwa kushughulikia tatizo la mrundiko wa taka katika kaunti hiyo.