Wakazi wa Gituamba na Makongeni wahofia kushambulia na majambazi kufwatia kukatizwa kwa umeme

Wakazi wa maeneo ya Gituamba na Makongeni huko Ruai katika kaunti ya Nairobi sasa wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na majambazi kufuatia tatizo la kukatizwa kwa umeme katika eneo hilo. Wakazi hao sasa wanasema wametoa habari kwa afisi za kampuni ya umeme ya Kenya Power zilizoko Ruai kuhusu tatizo hilo lililoanza ijumaa iliyopita, lakini hakuna hatua ambayo imechukuliwa. Mkazi Rose Nyaguthie alilieleza shirika la utangazaji nchini KBC kwa njia ya simu kwamba alipopiga simu katika afisi yas kampuni hiyo huko Ruai , mfanyikazi mmoja alimweleza kwamba tatizo hilo la umeme limetokana na transfoma iliyo na hitilafu, na kumshauri aendee nyingine katika afisi za kampuni hiyo huko Donholm au jijini. Inaarifiwa kwamba visa kadhaa vya kuzorota kwa usalama vimeripotiwa katika eneo hilo kutokana na tatizo hilo na sasa wakazi wanatoa wito kwa wasimamizi wa kampuni ya Kenya Power wachukue hatua. Walishangaa ni kwa nini kampuni hiyo haijawasilisha tranfoma nyingine siku tano baada ya tatizo la umeme kutokea katika eneo hilo huku wakiendelea kupata hasara. A�A�A�