Wakazi wa Ghouta nchini Syria waripotiwa kutoroka makwao kutokana vita

Wakazi walioko katika ngome ya waasi ya mashariki mwa Ghouta nchini Syria wanaripotiwa kutoroka eneo hilo huku hali katika eneo hilo ikitajwa kuwa mbaya zaidi . Wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo wanaonekana kupiga hatua katika harakati za kulinyakuwa eneo hilo lililoko karibu na eneo la Mashariki mwa mji mkuu wa Damascus. Kundi moja la kutetea haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema kuwa jeshi la A�serikali sasa linakaribia eneo hilo. Msafara wa magari ya kutoa msaada wa Umoja wa Mataifa uliotarajiwa kufika katika eneo hilo siku ya Jumapili haujaweza kuafikia lengo lake . Mapigano hayo ya tangu tarehe 18 mwezi Februari yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 600 wengi wao wakiwa watoto . Usitishaji wa mashambulizi kwa saa tano kila siku ulioagizwa na Urusi au agizo la baraza la usalama la umoja wa mataifa la kusitishwa kwa mashambulizi kote nchini humo hayajafanikiwa kuleta msaada wa kibinadamu katika ngome hiyo ya waasi. Takriban watu 393,000 wamekwama katika eneo hilo.