Wakaazi wa Salgaa waunga mkono ujenzi wa barabara ya safu mbili

Shinikizo zingali zinaendelea kwa taasisi zinazohusika kujenga barabara ya safu mbili katika eneo la Salgaa, huku wakaazi wa eneo hilo wakijitokeza wazi wazi kuunga mkono wazo hilo. Pendekezo hilo lilitolewa mara ya kwanza wiki mbili zilizopita na mamlaka ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama barabarani NTSA, ikisema hilo ndilo jawabu la pekee la kumaliza visa vingi vya ajali katika eneo la Salgaa; Sachanga��wan hadi Mau Summit, kwenye barabara kuu Nakuru kuelekea Eldoret. Wakaazi wa eneo hilo la Salgaa sasa wanasema kwamba taasisi zote za serikali hazina budi kushirikiana katika kuchunguza uwezekano wa kujenga barabara yenye safu mbili ili kuokoa maisha. Wiki moja iliyopita abiria-11 walipoteza maisha yao baada ya a�?Nissan Shuttlea�? waliyokuwa wakisafiria kugonga Nga��ombe katika barabara hiyo mwendo wa saa tisa usiku; akiwemo mtu mmoja na mkewe. Valentine Sitienei na Mumewe Jared Koskey walikuwa wamehudhuria hafla ya kufuzu kwenye chuo kikuu cha kilimo na teknolojia cha Jomo Kenyatta, Kaunti yaA�A�Kiambu, ambako Sitienei alikuwa amehitimu shahada ya Uzamili katika somo la usimamizi wa biashara kabla ya kufariki kwenye ajali katika barabara hiyo.