Wakaazi Baringo wataka serikali kuimarisha usalama

Wakazi wa Baringo wametoa wito kwa serikali itwae bunduki zote zinazomilikiwa kinyume cha sheria na watu wanaoshukiwa kuwa majangili wa ki Pokot. Kulingana na wakazi hao, hali ya usalama imezorota katika sehemu hiyo licha ya kupelekwa kwa maafisa wa usalama. Visa vya uvamizi na mashambulizi vinavyotekelezwa na majangili kutoka jamii ya WaPokot vimeongezeka licha ya oparesheni inayotekelezwa na maafisa wa usalama, jambo ambalo limesababisha shule kadhaa kufungwa. Viongozi wa kisiasa katika sehemu hiyo wametoa wito kwa serikali kutoa chakula cha msaada kwa familia zilizoathiriwa mbali na kuhakikisha usalama wao. Sehemu za Muchungoi, Chebinyin na Mukutani kwenye kaunti ya Baringo ndizo zimeathiriwa zaidi.