Wajumbe wa mabunge yote mawili wa Jubilee wapongeza juhudi za Rais Uhuru

Wajumbe kwenye bunge la kitaifa na wenzao katika bunge la Seneti kutoka chama cha Jubilee na pia vyama tanzu wamepongeza juhudi za Rais Uhuru Kenyatta za kuhakikisha usawa na pia amani miongoni mwa Wakenya. Wabunge hao waliokuwa wakiongea baada ya hotuba ya Rais kwa kikao cha pamoja cha mabunge yote mawili walisema kwamba Rais amejitoleaA� kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wanao-ishi na ulemavu, kina- mama, wakongwe na pia maeneo yaliyotengwa.A� Ma-Seneta Samuel Poghisio wa [Pokot Magharibi], Johnson Sakaja wa [Nairobi];A� mwakilishi wa wanawake katika kaunti yaA� Uasin Gishu Gladys Boss Shollei, Janet Nangabo wa [Trans Nzoia], Emmanuel WangweA� wa [Navakholo] na mwenzake wa Bura, Ali Wario, walisema kwamba makundi mbali mbali ya waliotengwa humu nchini sasa yanafurahia matunda ya kutengewa viti maalum, na pia mfumo wa utawala wa magatuzi. Aidha, walipongeza hatua ya Rais Uhuru Kenyatta, ya kukubali uamuzi wa mahakama ya juu, uliofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais wa tarehe 8 Augosti mwaka huu. Hata hivyo walisema kwamba Rais ana haki ya kuelezea kutoridhishwa kwake na uamuzi huo, kwani kufanya hivyo hakutabadili uamuzi huo wa mahakama ya juu. Wabunge wa upinzani walitimiza tishio laoA� la kuto-hudhuriaA� sherehe rasmi za ufunguzi huo na badala yake kuungana na viongozi wa (NASA) kwenye kampeini katika eneo bunge la Kibra.