Wajumbe Elfu 7 Wa Mrengo Wa Jubilee Wakongamana Nairobi

Wajumbe elfu-7 wa vyama sita tanzu vya mrengo wa Jubilee wanakongamana katika ukumbi wa Bomas of Kenya na kwenye uwanja wa Kasarani kuanzisha utaratibu wa kuvunjilia mbali vyama vyao kabla ya kuzinduliwa kwa chama kipya cha Jubilee. Hayo yanajiri huku usalama ukiimarishwa katika maeneo hayo. Vyama vinavyowakilishwa leo ni APK, TIP-TIP, United Democratic Forum, New Ford-Kenya, Jubilee Alliance (JAP) na Republican Congress. Baadhi ya wajumbe ambao hawakuwa na stakabadhi zinazohitajika walizuiliwa kuingia katika maeneo hayo. Wajumbe wa vyama vya URP, GNU na TIP wanakutana katika uwanja wa Kasarani pamoja na wale wa vyama vya The National Alliance (TNA) na Ford People.