Waititu Aangaziwa Kwa Kuongoza Vijana Kauharibu Mali Ya Thamani Ya Mamilioni

Mbunge wa Kabete, Ferdinand Waititu anaangaziwa kwa madai ya kuongoza kundi la vijana kuharibu mali ya thamani ya kibinafsi ya thamani ya mamilioni ya pesa huko Ndeiya, Limuru. Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi huko Limuru, Mohammed Bakuli, alisema wamepokea taarifa kutoka kwa watu mbali mbali walioshuhudia kisa hicho, na wanasubiri taarifa za mwisho ili waanze kuwakamata wahusika. Ardhi inayozozaniwa inadaiwa kuwa ya umma. Mwakilishi wa wadi ya Ndeiya, Nelson Munga, alikashifu kisa hicho, akisema mbunge huyo angepata ushauri kwanza kabla ya kuwatumia vijana hao ambao pia huenda wakakamatwa kwa kukiuka sheria.