Waiguru apuuzilia uwezekano wa kushauriana na wauguzi wanaogoma

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru amepuzilia mbali uwezekano wa kushauriana na wauguzi wanaogoma akisema wale wanaotaka kuhifadhi nafasi zao lazima watume upya maombi ya kazi. Waiguru anasema taasisi ya serikli iliyo na jukumu la kushughulikia malalamishi ya wauguzi tayari imefanya uamuzi wake ilhali mahakama imeamulu kuwa mgomo huo si halali. Akiongea wakati wa ufunguzi wa bunge la kaunti hiyo, Waiguru aliwahimiza wauguzi wanaogoma kurejea kazini akisema serikali ya kaunti hiyo itazingatia azimio la baraza la magavana la kuwaajiri wauguzi wapya kuhakikisha huduma za matibabu zinarejelewa katika hospitali za umma.