Waiguru ahojiwa na tume ya EACC

Waziri wa ugatuzi anayekumbwa na mzogo, Anne Waiguru kwa sasa yuko katika afisi za tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi kuangazia zaidi kuhusu madai ya ufisadi katika wizara yake.

Tume ya EACC ilimuagiza Waiguru kufika mbele yake kwa mahojiano na kuandikisha taarifa kuhusu kupotea kwa karibu shilingi bilioni moja katika shirika la vijana wa huduma kwa taifa-NYS. Hapo jana, katibu wa mipango, Peter Mangiti aliitisha mkutano wa wanahabari stakabadhi alizowasilisha kwa kamati ya bunge kuhusu uhasibu wa fedha za umma ambazo ziliangazia bei za juu kupita kiasi ya bidhaa zilizonunuliwa.

Awali, alikuwa amehojiwa kwa zaidi ya saa nane na wapelelezi wa tume ya EACC kuhusu kashfa iliyokumba shirika ka NYS. Akijitetea Waiguru alikanusha kuhusika katika sakata hiyo na kuwalaumu maafisa wa uhasibu katika wizara yake.

Kadhalika amewalaumu wakosoaji wake kwa kutoa matamshi ya kumchafulia sifa licha ya kwamba yeye si afisa wa uhasibu na hajawahi kuhusika katika ununuzi wa bidhaa zinazodaiwa kununuliwa kwa bei ya juu kupita kiasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *