Wahudumu Wa afya Watishia Kugoma Nyandarua

Wahudumu wa afya katika kaunti ya  Nyandarua wametishia kugoma iwapo serikali ya kaunti hiyo itakosa kulipa marupurupu ya mishahara yao iliyocheleweshwa kufikia saa sita usiku leo. Wakiongozwa na katibu wa chama cha wauguzi hapa nchini tawi la  Nyandarua Geoffrey Gachara, wahudumu hao wameshtumu serikali ya kaunti ya kaunti hiyo kwa kutotimiza ahadi yake ya kuwalipa. Gachara amesema serikali ya kaunti hiyo iliahidi kuwalipa kupitia aorodha maalum ya malipo wiki ya kwanza ya mwezi huu lakini haikufanya hivyo. Akiongea kwa njia ya simu kutoka mji wa Ol Kalou, Gachara  amesema ahadi ya kulipa pesa hizo pamoja na mishahara ya mwezi huu haitawezekana kwa sababu shughuli ya kutayarisha orodha ya malipo imeanza tayari . Amesema wahudumu hao hawana jingine ila kulemaza sekta ya afya katika kaunti hiyo. Hayo yamejiri huku rais  Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuzuru eneo hilio Jumamosi hii.