Wahudumu Wa Afya Wagoma

Wahudumu wa afya leo asubuhi wametekeleza tisho lao la kugoma, kushinikiza kutekelezwa kwa makubaliano ya mazungumzo ya mwaka wa  2013.Uchunguzi uliofanywa na shirika la utangazi la  KBC ,umebainisha kuwa hospitali nyingi hazina wahudumu hao. Huko  Nanyuki, hospitali ya rufaa ilikuwa imefungwa huku walinda usalama wakiwarejesha nyumbani wagonjwa waliokuwa wakitafuta huduma za matibabu.   Hospitali hiyo ya rufaa ambayo uhudumia wagonjwa kutoka kaunti za Laikipia, Nyeri, Meru na  Isiolo,kwa kawaida huwa na shughuli nyingi siku za jumatatu .Katika kaunti ya embu  Seneta lenny Kivuti  ameihimiza serikali kutekeleza makubaliano hayo ,ili kumaliza mzozo katika sekta ya afya .Kulingana na mujibu wa seneta huyo ,serikali haifai kufanyia mzaha maisha ya wakenya.