wahamiaji 91kutoka Iraq na Syria wakamatwa nchini Romania

Maafisa wa kushika doria kwenye mpaka wa Romania wamewapata wahamiaji-91 kutoka Iraq na Syria waliojificha kwenye lori lililokuwa likisafirisha vipuri vya magari. Waliwafahamisha polisi kwamba walikuwa wakijaribu kufika katika eneo huru la usafiri la Schengen. Polisi walipekua gari hilo lililokuwa na nambari za usajili za Uturuki katika kituo cha kuvukia mpakani nchini Hungary hapo jana. Kulingana na stakabadhi zilizopatikana, lori hilo lilikuwa likisafirisha vipuri hivyo vya magari hadi nchini Norway. Dereva wa lori hilo aliwaambia maafisa wa serikali ya Romania kwamba hakufahamu kuhusu wahamiaji hao. Wahamiaji hao wanachunguzwa kwa tuhuma za kujaribu kuvuka mpaka kinyume cha sheria huku dereva huyo akishukiwa kuwa mshirika wao.