Wagombeaji Saba Waidhinishwa na Tume ya IEBC Kuwania Kiti Cha Malindi

Tume huru ya uchaguzi na mipaka a��IEBC imewaidhinisha wagombezi saba kuwania kiti cha ubunge cha Malindi kwenye uchaguzi mdogo wa tarehe 7 mwezi ujao.Wagombezi wawili Fuad Kombe wa Kanu na Farhan Mohamed wa chama cha Maendeleo Democratic hata hivyo walijiondoa kwenye uchaguzi huo kutokana na kile walitaja kuwa ukosefu wa pesa za kufanya kampeini. Wagombezi watano waliwasilisha karatasi zao za uteuzi siku ya jumatatu na wengine wawili siku ya jumanne.Mgombeaji wa ODM Willy Mtengo,Attas Sharrif Ali wa LPK,Philip Charo wa JAP ,David Mangi wa Shirikisho na Nelson Gunga wa Ford-People waliwasilisha karatasi zao siku za jumatatu.