Wagombea urais kupewa fursa ya kuuza sera zao kwenye mijadala ya runinga

Wagombea urais hapa nchini watakuwa na fursa ya kuuza sera zao kwa mamilioni ya Wakenya wakati wa mijadala ya runinga itakayopeperushwa na vituo vyote vya utangazaji kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Mijadala hiyo ambayo ni ya pili kuandaliwa tangu kuratibishwa kwa katiba mpya itafanyika katika awamu tatu ambapo wagombea wenza pia watashiriki kwenye mijadala hiyo ya runinga. Mijadala hiyo itapeperushwa moja kwa moja na vituo vyote vya redio na runinga pamoja na mitandao ya kijamii kati ya tarehe 10 na 27 mwezi Julai mwaka huu.Mijadala hiyo inanuiwa kuwasaidia wapiga kura kufanya maamuzi wa busara na pia kuimarisha utangamano wa taifa. Kamati ya wadau katika sekta ya vyombo vya habariwanakamilisha sheria za kutoa mwongozo wakati wa mijada hiyo ikitiliwa maanani idadi kubwa ya wawaniaji wanaoazimia kugombea urais. Wakenya 18 watagombea urais kwenye uchaguzi mkuu mwezi Agosti, ikiwa wataishinishwa naA� tume ya IEBC baada ya kupokea idhini kutoka kwa msajili wa vyama vya kisiasa. Kati ya wagombea hao 18, saba watawania kwa tiketi ya vyama tofauti ilhali hao wengine waliosalia watawania uchaguzi huo kama wagombea huru. Mjadala huo utaandaliwa katika chuo kikuu cha Afrika mashariki cha kanisa katoliki.