Wafungwa Wa Geraza La Guantanamo Kuhamishwa Ili Kufanikisha Kufungwa Kwa Gereza Hilo

Makao makuu ya Pentagon yapanga kuwahamisha wafungwa kutoka gereza la Guantanamo hadi katika mataifa mawili ambayo yamekubali kuwachukuwa na kuwahifadhi. Hii ndio hatua ya mwisho ya juhudi za rais wa Marekani Barack Obama za kujaribu kufunga gereza hilo. Afisa mmoja wa Marekani amesema kuwa kuhamishwa huko kunatarajiwa kufanywa katika muda wa siku kadhaa zijazo. Miongoni mwa wafungwa hao ni raia mmoja wa Yemen Tariq Ba Odah ambaye alikuwa katika mgomo wa chakula na akapoteza nusu ya uzani wake wa mwili. Kuna takriban wafungwa 91 katika gereza hilo lililoko huko Cuba.