Wafula Chebukati Asailiwa na Kamati ya Bunge

Wafula Chebukati ambaye amependekezwa kuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka -IEBC A�leo asubuhi alisailiwa na kamati ya bunge la kitaifa kuhusu maswala ya sheria. Chebukati aliliambia jopo hilo la usaili kuwa ana tajriba ya kuongoza tume hiyo na kwamba atatekeleza majukumu yake bila mapendeleo wala hofu. Chebukati alisema ataangazia ubunifu ili kuwezesha tume hiyo kushughulikia maswala yote kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ya kijamii. Alisema kuna mambo ambayo wakenya walijifunza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 ikiwemo maeneo yanayokumbwa na machafuko kutokana na madai ya visa vya udanganyifu na swala hilo linapaswa kushughulikiwa katika uchaguzi mkuu ujao. Bunge la kitaifa ambalo kwa sasa liko mapumzikoni lina muda wa siku saba kumsaili Chebukati na watu wengine sita waliopendekezwa na rais Kenyatta kuwa makamishna wa tume ya IEBC. Chebukati amekuwa wakili kwa zaidi ya miakaA�A�29 na ni mshirika mkuu kwenye kampuni ya mawakili ya Cootow.