Wafugaji wa Kajiado kunufaika na mradi wa kuchimba visima

Serikali ya kaunti ya Kajiado ikishirikiana na serikali ya kitaifa inachimba visima zaidi katika eneo hilo kwa manufaa ya wafugaji. Kati ya visima hivyo, kimoja kinaweza kutoa lita elfu 6 za maji katika eneo la Ilonamen Mashuru kunufaisha wafugaji elfu 5. Maji yamekuwa chanzo cha mzozo miongoni mwa wakazi wa Kajiado. Kwingineko A�benki ya Equity imezindua tawi lake jipya katika mji wa Unguja.A�Tawi hilo la Unguja linafikisha 14 idadi ya matawi ya benki ya Equity nchini Tanzania kama sehemu ya mpango wa benki hiyo wa kuongeza idadi ya matawi yake katika kanda hii. Hatua ya Equity ya kufungua tawi lake jipya huko Zanzibar inatarajiwa kuimarisha huduma za benki hiyo kwa wateja wake katika eneo hilo. Waziri wa fedha na mipango wa Unguja, daktari Khalid Salum Mohamed alisifu hatua hiyo akisema itahimiza maendeleo.