Wafuasi Wa Cord Wakita Kambi Mjini Kilifi Kabla Ya Ziara Ya Raila

Mamia ya wafuasi wa muungano waA� cord wamekita kambi katika uwanja waA�Karisa Maitha mjini Kilifi kabla ya ziara ya kiongozi wa muungano huo Raila Odinga katika kaunti hiyo leo alasiri . Kabla ya kuandaa mkutano katika eneo hilo Raila anatarajiwa kuwahamasisha wafuasi wake huko Mtwapa kujisajili kuwa wapiga kura kwenye shughuli ya kusajili wapiga kura inayoendelea.A� Kigogo mwenzaA� Kalonzo Musyoka pia leo alasiri anatarajiwa kuzuru kaunti zaA� Kitui na Makueni kwa shughuliA� sawia. Kwingineko kaunti ya Embu imesambaza zaidi ya makarani A�10,000 ili kusaidia katika shughuli ya kusajili wapiga kura. Seneta wa kaunti hiyo Lenny Kivuti amesema analenga kuhamasisha usajili wa zaidi ya wapiga kura wapya laki mbili katika kaunti hiyo. Kivuti ambaye pia anawania kiti cha ugavana cha kaunti ya A�Embu kwa tikiti ya chama cha Jubilee amesema makarani hao watafanya uhamasishaji wa nyumba hadi nyumba. Kwingineko naibu kamishna wa kaunti ya Kiambu A�Tom Anjere amewatahadharisha machifu na manaibu wao wanaodaiwa kuitisha hongo ili kutoa vitambulisho vya kitaifa kwa wakenya . Amesema maafisa hao watashtakiwa. Akiwahutubia wanahabari baada ya kukagua shughuli katika kituo cha Huduma Centre cha kaunti hiyo Anjere alisema zaidi ya vitambulisho A�2500 vya kitaifa havijachukuliwa na wenyewe katika kituo hicho na kuhimiza wamiliki wa vitambulisho hivyo kuvichukua mara moja.