Wafanyikazi wawili wa shirika la ndege nchini Kenya Airways wakamatwa

Wafanyikazi wawili wa shirika la ndege nchini a�?Kenya Airwaysa�? walikamatwa jana asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakiwa na karibu kilo 20 za bidhaa iliyoaminika kuwa mihadarati. Wafanyikazi hao walikuwa wameabiri ndege kuelekea Cotonou, Benin, wakati waliponaswa. Kulingana na mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na mihadarati Hamisi Masa, wawili hao walikamatwa jana walipokuwa wakijiandaa kuabiri ndege ambayo iliondoka jana saa mbili asubuhi kuelekea Afrika Magharibi. Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, shirika la ndege la a�?Kenya Airwaysa�? lilisema limefahamishwa juu ya kisa hicho na kwamba linashirikiana na taasisi husika katika kutafuta suluhu. Hicho kilikuwa kisa cha pili katika muda usiozidi mwezi mmoja, ambacho kimehusisha wafanyikazi wa A�shirika la a�?Kenya Airwaysa�? baada ya wafanyikazi wengine wawili kushikwa na madawa walipokuwa wanapanga kusafiri hadi China. Aidha, Hamisi alisema polisi wameimarisha uchunguzi katika uwanja huo wa ndege, baada ya kufahamika kwamba ulanguzi unatekelezwa kwa kushirikiana na wafanyikazi wa a�?Kenya Airwaysa�?.