Wafanyikazi wa shughuli za dharura Ethiopia waendelea kutafuta miili ya watu kutoka jaa la taka

Wafanyikazi wa shuguli za dharura katika jiji kuu nchini Ethiopia kwa siku ya tano mfululizo wameendela kutafuta miili ya watu kutoka kwenye jaa la taka huku idadi ya waliofariki ikiongezeka na kufikia 115. Miili miwili zaidi iliondolewa leo asibuhi iku moja baada ya msemaji wa serikali kutangaza kuwa watu waliofariki ni 113 wakiwemo wanawake 75. Raia katika eneo hilo wamesemaA�A�yamkini watu themanini hawajulukani waliko. Badhi ya wahasiriwa wamezikwa hadi kufukia sasa katika shamba lililo karibu na kanisa la Abune Aregawi. Taifa hilo la upembe wa Afrika limetangza siku tatu za kuomboleza waliofariki siku ya Jumamosi katika mkasa huo kwenye jaa la taka ambalo limekuwepo kwa muda wa miaka hamsini.