Wafanyikazi saba wa jarida la Uganda washtakiwa kwa kumharibia sifa Museveni

Wafanyikazi saba wa jarida la Uganda la A�Red Pepper tabloid wakiwemo wahariri wake wakuu wameshtakiwa kwa kumharibia sifa rais Yoweri Museveni, ndugu yake jenerali Salim Saleh na waziri wa usalama A�Henry Tumukunde. Waendesha mashtaka A�wanadai kuwa washtakiwa ambao wanazuiliwa korokoroni waliwaharibia sifa watatu hao kufuatia uchapishaji wa taarifa kwa mada A�: a�?M7 plots to overthrow Kagame – Rwandaa�?. Jarida hilo halijasema lolote kuhusiana na swala hilo. Baada ya habari hizo kuchapishwa tarehe 20 mwezi Novemba waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa taifa hilo alizipuuza na kusema hazikuwa na nia njema na zililenga kuyagonganisha mataifa ya Uganda na Rwanda yanayoongozwa na rais Museveni na rais Paul Kagame mtawaliwa.