Wafanyibiashara wakadira hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa

Mamia ya wafanyibiashara katika kituo cha mabasi cha Ngara jijini Nairobi wanakadiria hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa na askari wa serikali ya kaunti ya Nairobi leo asubuhi. Idara ya ukaguzi wa mijengo katika jiji la Nairobi ilivamia eneo hilo leo asubuhi na kubomoa vibanda vyote vilivyojengwa kwa njia isiyohalali katika hatua iliyowaacha wafanyibiashara hao vinywa wazi. Mkurugenzi wa shughuli katika idara hiyo,A�Peter Mbaya,A�alisema vibanda hivyo vilibomolewa baada ya kumalizika kwa ilani ya miezi mitatu. Alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kupanua kituo hicho cha mabasi kwa lengo la kumaliza msongamano wa magari katikati ya jiji.