Wadau kuamua iwapo shule zitafungwa tarehe 17 Octoba

Uamuzi mkubwa kuhusu iwapo au la shule zifungwe wakati wa wiki ya uchaguzi mpya wa urais utaamuliwa wakati wa mkutano wa wadau wa elimu hivi leo. Mkutano huo utawaleta pamoja maafisa kutoka Baraza la mitihani nchini, Taasisi ya maendeleo ya mitaala, Wizara ya Elimu na wakuu wa shule za sekondari na shule za msingi na kuangalia hatua kadhaa.

Hatua moja ni kufunga shule zote wakati wa uchaguzi hapo Oktoba 17 ama kufunga shule zisizizokuwa za mabweni na kuruhsu shule zenye mabweni kuendelea na shughuli zao. Shule zilizofunguliwa kwa muhula wa tatu hapo Agosti 28 na kufungwa Oktoba 29 ili kuruhusu kuanza kwa mitihani ya kitaifa. Muhula wa tatu ni wiki tisa pekee na shughuli kama vile maombi na siku za kuwatembelea wanafunzi shuleni, mapumziko mafupi ya wanafunzi, michezo, hafla za utoaji tuzo na mikutano mikuu ya kila mwaka hairuhusiwi ili kukatiza mawasiliano kati ya watahiniwa na watu kutoka nje.