Wachunguzi watumwa Kenyatta kufwatia madai ya ubakaji wa wagonjwa

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa maswala ya jinaiA�A�George Kinoti ametuma kundi maalum la wachunguzi katika hospitali ya kitaifa yaA�A�Kenyatta ili kuchunguza madai ya ubakaji na kunyanyaswa kwa wagonjwa. Kwa mujibu wa Kinoti, kundi hilo linaA�A�wachunguzi waliobobea kutoka vitengo mbalimbali kutoka idara hiyo na wengine kutoka idara ya jinsia na maswala ya watoto kutoka huduma ya polisi.

Wakati huo huo, kufuatia madai ya ubakaji yaliyoigubika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta juma hili, kundi moja la wanawake kutoka eneo bunge la Kibra ambapo hospitali hiyo inapatikana wametoa wito wa kufanywa kwa uchunguzi wa haraka ili kubaini usuli wa swala hilo. Hospitali hiyo hupokea maelfu ya wagonjwa hasa kutoka mtaa wa mabanda wa Kibera. Wakiongozwa na Hamida Twahir, wanawake hao wametoa wito kwa wasimamizi wa hospitali hiyo kuunganisha maeneo ya kukuza watoto waliozaliwa kabla ya muda wao kutimia na lile la kujifungua akina mama.A�A�Walisema kuwa madai hayo ya ubakaji yanarejesha nyuma kujitolea kwa serikali kutoa huduma bora za afya.A�A�Kundi hilo la wanawake limetoa changamoto kwa waziri wa afya Cleopa Mailu kuhakikisha kuwa akina mama wote wanaonyonyesha katika hospitali hiyo wanawekwa katika orofa ya kwanza.