Wachezaji Wanne Wanaochezea Timu Za Kimataifa Kujiunga Na Harambee Stars Mazoezini

Wachezaji wanne wanaochezea timu za kimataifa;Jesse Were, Anthony Akumu, David Owino anayekichezea kilabu cha Zesco United nchini Zambia na Aboud Omar anayechezea timu ya A�Bulgaria wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya soka Harambee Stars mazoezini; huku Kenya ikijiandaa kwa mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Sudan. Aidha,wachezaji hao waliwasili humu nchini mapema leo baada ya safari ndefu kutoka vilabu wanavyochezea. Kenya itakabiliana na Sudan katika mechi ya kirafiki Ijumaa hii kisha ipimane nguvu na Tanzania siku ya Jumapili tarehe 29 mwezi huu katika uwanja wa michezo wa kimataifa wa Moi Kasarani, jijini Nairobi. Mechi hizi ni za kuandaa timu ya Kenya kwa mechi ya Kundi a�?Ea�� ya kufuzu kwa kombe la Bara Afrika dhidi ya Kongo Brazzaville, tarehe tano mwezi Juni.