Wachezaji wa Kenya waanza mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Tenisi ya wachezaji wanaotumia viti vya magurudumu

Wachezaji wa Kenya wameanza mazoezi kabambe katika kilabu cha Nairobi kujiandaa kwa mashindano ya tenisi ya wachezaji wanaotumia viti vya magurudumu yatakayoanza mwishoni mwa mwezi ujao nchini Naijeria.

Wachezaji wanne wa tenisi ya kutumia viti vya magurudumu wamedhibitisha kushiriki katika mashindano ya kombe la “Naijeria Open” ya shirikisho la wachezaji tenisi wa kulipwa nchini humo kuanzia tarehe 31 mwezi ujao hadi tatu mwezi wa kumi na moja, mwaka huu.

Wachezaji hao ni: Jane Ndenga, Phoebe Masika, Peter Munuve na Collins Omondi. Aidha, wachezaji hao wameapa kufanya vyema nchini Naijeria ili wafuzu kwa michuano ya “Dan Devan” itakayoanza tarehe tano hadi nane mwezi Novemba, nchini Ghana.