Wabunge Watatu Wafika Mbele Ya Maafisa Wa Upelelezi Kusailiwa Kuhusiana Na Matamshi Ya Chuki

Wabunge watatu walifika mbele ya maafisa wa idara ya upelelezi ili kusailiwa kuhusiana na matamshi ya chuki. Kwenye taarifa inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet alimuagiza mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, Kimani Ngunjiri wa Bahati na Ferdinand Waititu wa Kabete wafike kwenye afisi za idara hiyo kutokana na matamshi ya chuki waliyoyatoa. Wengine wanaokabiliwa na mashtaka sawa na hayo ni mbunge Timothy Bosire wa Kitutu Masaba, Junet Mohamed wa Suna Mashariki, Seneta wa Machakos Johnson Muthama na mwakilishi wa wanawake huko Kilifi Aisha Jumwa ambao bado hawajafika kwenye afisi za idara hiyo.

Mwenyekiti wa Tume ya uwiano na mshikamano wa kitaifa Francis Ole Kaparo alisema watawataka Kuria na Ngunjiri kuandikisha taarifa kwenye afisi hizo na A�kuitaka mahakama kukatalia mbali ombi la dhamana A�lililowasilishwa mahakamani na Kuria kuhusiana na kesi nyingine. Kuria alitioa matamshi ya kutaka kiongozi wa muungano wa CORD Raila Odinga auawe.

A�