Wabunge Walioshikwa kwa Madai Ya Kutoa Matamshi Ya Chuki Wangali Korokoroni Kwa Siku Ya Pili

Wabunge wanane waliokamatwa siku ya jumanne kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki walisalia korokoroni jana kwa siku ya piliA�kwenye vituo mbali mbali vya polisi jijini Nairobi.A�Hii ni baada ya ombi lao la kutaka waachiliwe kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea kukataliwa na mahakama..Wabunge hao akiwemo seneta wa kaunty ya Machakos, Johnson Muthama na wabunge Junet Mohamed, Aisha Jumwa, Timothy Bosire, Florence Mutua.Wanadai waliagizwa kufika katika makao makuu ya CID bila arifa ya kuwataka wafike katika kituo chochote cha polisi.Kupitia kwa mawakili wao, wanasema wamezuiwa kwa masaa kadhaa bila chakula, maji wala huduma za matibabu.Pia wanasema hawajakubaliwa kuwaona jamaa zao au wake wao.Wamemshtaki ispekta generali wa Polisi na mkurugenzi wa mashtaka ya uma na mkurugenzi wa C.I.D. Viongozi hao wanaozuiliwa katika vituo vya polisi vya Pangani na Muthaiga wanahofia kwamba huenda wakaendelea kuzuiwa, hatua inayokiuka haki zao.Mahakama iliagiza wabunge hao wa CORD wazuiwe korokoroni hadi ijumaa tarehe 17 mwezi huu pamoja na wabunge Moses Kuria, Ferdinand Waititu na Kimani Ngunjiri wa muungano wa jubillee ambao pia wanakabiliwa na mashtaka ya kutoa matamshi ya chuki.