Wabunge waliochaguliwa hivi majuzi wahudhuria mafunzo ya wiki moja

Wabunge waliochaguliwa hivi majuzi wanahudhuria mafunzo ya wiki moja kujifahamisha taratibu na kanuni za bunge. Kulingana na katibu wa bunge la kitaifa, Michael Sialai mafunzo hayo yanafanyika katika hoteli moja jijini kabla ya kikao cha pamoja cha bunge hapo kesho ambacho kitahutubiwaA� na rais Uhuru Kenyatta. Sialai aliongeza kuwa wabunge hao wanahamasishwa kuhusu wajibu wao wa kikatiba yakiwemo majukumu yao katika bunge, maswala ya uongozi, utayarishaji bajeti na muundo wa kamati mbali mbali za bunge. Baadaye hii leo, waakilishi wa idara mbali mbali za umma watawahutubia wabunge hao. Hafla hiyo pia itatoa fursa kwa wabunge hao kutangamana na kubadilishana mawazo na washiriki wa asasi nyingine za umma pamoja na sekta ya kibinafsi. Wabunge hao pia watatumia fursa hiyo kuwasilisha takwimu zao kwa afisi tofauti za bunge la kitaifa.