Wabunge Wakatalia Hoja Ya Kubuni Kamati Ya Bajeti.

Wabunge jana walikatalia hoja ya kubuni kamati ya bajeti na ugavi wa fedha. Spika wa bunge la taifa Justin Muturi hata hivyo akitumia A�kanuni nambari moja ya bunge, aliziagiza kamati zote husika za bunge kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu bajeti , akisema utaratibu wa kutayarisha bajeti sharti uendelee hata bila kuwepo kwa kamati hiyo ya bajeti.