Wabunge Wa Uganda Kujitolea Kufadhili Uganda Cranes

Wabunge wa Uganda watatoa asilimia moja ya mshahara wao wa mwezi Januari kusaidia timu ya taifa hilo Uganda Cranes kushiriki katika fainali za kombe la bara Afrika nchini Gabon. A�Spika wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga A�alisema kuwa kila mbunge atatoa jumla ya shilingi elfu 15 pesa za humu nchini A�na wanalenga kuchangisha jumla ya shilingi milioni sita pesa za humu nchini. A�Timu hiyo ya Cranes, A�inayofunzwa na Milutin Sredojevic, kwa sasa iko katika Milki za Kiarabu ambako inatarajiwa kuchuana na Kodivaa katika mechi yao ya mwisho ya kirafiki ya kimataifa leo kabla ya kuondoka kwenda Gabon.A� A�Uganda, A�iliyofuzu kwa fainali hizo kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 39, itacheza mechi zake za makundi A�kwenye fainali hizo zitakazoandaliwa baina ya tarehe 14 mwezi huu na tarehe 5 mwezi ujao mjini Port-Gentil. Timu hiyo itafungua kampeni zao kwa mechi dhidi ya Ghana tarehe 17 Januari.A� A�Timu nyingine katika kundi a�?Da�� A�ni A�Mali na Misri.