Wabunge wa NASA na maafisa wa idara ya mahakama wasusia ufunguzi wa bunge

Wabunge wengi wa muungano wa (NASA) na pia maafisa wa idara ya mahakama walisusia shughuli rasmi ya ufunguzi wa bunge,A� ambayo iliongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Ni mbunge mmoja pekee anayeegemea muungano huo wa NASA a�� hususan Mbunge wa Webuye Masahriki Alfred Sambu wa chama cha Amani National Congress-(ANC), ambaye alihudhuria hafla hiyo. Waakilishi wa idara ya mahakama pia walisusia hafla hiyo ijapo walikuwa wametengewa viti. Hata hivyo, wabunge waliochaguliwa bila kuegemea chama chochote walihudhuria sherehe hizo.A� Aidha, Ma-waziri ikiwa ni pamoja na Najib Balala wa (Utalii), Eugene Wamalwa wa (Maji), (kaimu waziri wa usalama wa kitaifa)- Fred Matiang’i, Henry Rotich wa (Fedha), Mwangi Kiunjuri wa (Ugatuzi) na pia maafisa mbali mbali wa ngazi za juu serikalini walihudhuria sherehe hizo. Viongozi wa kidini ambao walihudhuria sherehe hizo ni pamoja naA� Askofu mkuu Jackson Ole Sapit wa kanisa laA� Anglikana, ambaye alianza kwa maombi yaliyogusia amani wakati wa marudio ya uchaguzi wa Urais tarehe 17 Octoba mwaka huu.