Waathiriwa Wa Utekaji Nyara Wa Ndege La Misri Wawasili Mjini Cairo

Abiria na wafanyakazi wa ndege ya shirika la ndege la Misri iliyokuwa imetekwa nyara wamewasii mjini Cairo kutoka Cyprus huku nia hasa ya mtekaji nyara ikiwa bado haijulikani. Abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo waliwasili jana usiku jijini Cairo baada ya mtekaji nyara huyo kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Alexandria kuelekea Cairo wakati mtekaji nyara alipoiamuru kelekea nchini Cyprus jana asubuhi. Mtekaji nyara huyo alikuwa amejifunga ukanda bandia wa vilipuzi huku akitishia kulipua ndege hiyo. Watu themanini na mmoja wakiwemo wageni-21 na wafanyakazi-15 walikuwa kwenye ndege hiyo aina ya Airbus 320. Raia wengi wa Misri waliangazia tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii lakini abiria walisema walihofia maisha yao.