Waandamanaji Wa CORD Walemaza Shugli Za Kibiashara Katika Kaunti Za Kisumu,Migori

Shughuli za biashara katika kaunti za Kisumu na Migori zimesalia kufungwa leo asubuhi kwa hofu ya kutokea kwa visa vya wizi wa bidhaa kufuatia tangazo la muungano wa CORD kuwa ungerejelea maandamano yao ya kila wiki. Imesemekana waandamanaji walifunga barabara kwa mawe huku wakichoma magurudumu hata baada ya polisi wa kupambana na fujo kupelekwa katika kaunti za A�Migori, Kisumu na A�Nairobi kuzuia maandamano hayo ambayo polisi walitangaza jana kuwa haramu kabla ya tangazo hilo kupuziliwa mbali A�na mahakama leo asubuhi. Katika baadhi ya maeneo wazazi walihimizwa kutopeleka watoto wao shuleni . Shule ya msingi ya Olympic mtaani A�Kibera imesalia kufungwa leo. Viongozi wa Cord walikaidi tahadhari za awali na kuendelea na maandamano ya kila wiki ya kushinikiza kuondolewa afisini kwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka A�IEBC .