Waandamanaji wasababisha msongamano Voi

Polisi mjini VoiA� walikabiliana na mamia ya waandamanajiA� jana ,huku wakifungaA� barabara kuu ya Mombasa hadi Nairobi wakilalamikia swala la wageni kuajiriwa kazi kwenye kituo cha stesheni ya reli ya SGR badala ya wazawa wa sehemu hiyo.Makabiliano hayo yalisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo kuu,wakati vijana wasio na ajira waliokuwa na ghadhabu wakichoma tairi na kufunga barabara hiyo.Mandamano hayo yalianza pale vijana walipofika kwenye kituo cha treni cha Kasarani kuajiriwa kazi na badala yake wakajikuta wanafanyishwa kazi duni.Miongni mwa kazi walizokuwa wameahidiwa ni upishi,uanaskari na mafundi wa ukarabati.Vijana hao walimiinika barabarani na kuandamana huku wakiitaka kampuni hiyo kutowaajiri vijana kutoka nje ya sehemu hiyo.Polisi waliokuwa naA� silaha ,wakiwemo wale wa utawala walipelekwa katika sehemu hiyo na kuwatimua waandamanaji hao.Akiongea na wanahabari katika kituo cha treni cha Voi afisa mkuu wa polisi katika sehemu hiyo Joshua Chesire aliwakosoa waandanmanaji hao kwa kufunga barabara kuu na kutatiza wasafiri huku akisema jambo hilo haliwezi kutatua malalamishi yao.

A�