Waakilishi wa upinzani wajiondoa kwenye majadiliano kati ya IEBC na Jubilee

Waakilishi wa upinzani kwenye majadiliano kati yao na tume ya IEBC na chama cha Jubilee wamejiondoa. Akiwahutubia wanahabari nje ya ukumbi wa Bomas Seneta wa Siaya James Orengo alisema juhudi za chama cha Jubilee za kufanyia marekebisho sheria ya uchaguzi zinahitilafiana na lengo la mashauriano hayo. Alisema muungano wa NASA utakiachia chama cha Jubilee uhuru wa kufanya chochote kitakacho akisema kuwa juhudi za chama hicho za kubadilisha sheria ya uchaguzi ni jaribio la kuhalalisha kauli ya majaji wawili waliopinga uamuzi wa kubatilishwa matokeo ya uchaguzi wa urais.