Waakilishi wa Kenya waendeleza rekodi yao ya kutoshindwa kwenye mchuano wa mpira wa wavu

Waakilishi wa Kenya, Kenya Prisons na Kenya Pipeline waliendeleza rekodi yao ya kutoshindwa kwenye michuano ya mpira wa wavu ya kuwania kombe la Bara Afrika baina ya vilabu vya wanawake baada ya kuzishinda timu za Asec Mimosa ya Kodivaa na Vision ya Uganda; huku mashindano hayo ya Bara Afrika yakiingia siku ya pili jana jijini Kairo, Misri.

Waliokuwa mabingwa wa Bara Afrika, Kenya Prisons walianza harakati za kuwania taji ya Bara Afrika kwa ushindi wa seti tatu kwa sifuri dhidi ya Customs ya Naijeria. Prisons iliendeleza msururu wa matokeo bora kwa kuishinda Asec Mimosa ya Kodivaa kwenye mechi yake ya pili seti tatu kwa bila. Timu ya Prisons ilishinda seti ya kwanza alama 25 kwa 7 kisha ikanyakua seti zilizosalia alama 25 kwa 17 na 25 kwa 12. Kwa upande mwingine, wana-Pipeline wa Kenya waliilemea Vision ya Uganda seti tatu kwa moja: 25 kwa 7, 24 kwa 26, 25 kwa 13 na 25 kwa 15.A�A�Kwenye mechi nyingine,A�A�wenyejiA�A�El ShamsA�A�ya MisriA�A�waliinyuka Vision ya Uganda seti tatu kwa moja, Rwanda Revenue Authority ikaishinda NyongA�A�ya KameruniA�A�seti tatu kwa moja, hukuA�A�Bafia ya Kameruni ikiipikuA�A�Chlef ya Aljeria seti tatu kwa nunge.