Waakilishi wa Kenya kwenye mashindano ya tenisi wasuasua kwenye mashindano ya Bara Afrika

Waakilishi wa Kenya kwenye mashindano ya Bara Afrika ya tenisi ya mezani, Brian Mutua A�na Sejal Thakkar, walisuasua A�katika A�siku ya kwanza ya A�michuano hiyo jana katika ukumbi wa Kasarani wa michezo ya ndani. A�Mutua alishindwa kutamba mbele ya Idowu Saheed wa Kongo alipolemewa seti tatu kwa bila; naye Thakkar akasalimu amri dhidi ya Kessaci Katia wa Aljeria kwa idadi ya seti sawa na hizo kwenye mechi zao za ufunguzi. Mutua akishiriki kwa mara ya kwanza mashindanoni; alitwaa ushindi katika seti ya kwanza alama 11 kwa 8. Hata hivyo, Idowu alicheza kwa kujituma na kushinda seti ya pili alama 11 kwa 5, seti ya tatu alama 11 kwa 3 na kukamilisha seti ya nne kwa ushindi wa alama 11 kwa 6. Kwenye mechi nyingine, mchezaji anayeorodheshwa wa kwanza mashindanoni Omar Assar wa Misri, alimlemea Sultan Godfrey wa Ushelisheli seti tatu kwa sifuri, A�Derek Abrefa A�wa Ghana akampiku Kurt Lingeveldt wa Afrika Kusini seti tatu kwa moja naye Aruna Quadri wa Naijeria akamnyuka A�Nyoh Ofon Derek wa Kameruni seti tatu kwa yai. Katika kitengo cha akinadada, Mkenya A�Sejal Thakkar alilemewa na Kessaci Katia wa Aljeria seti tatu kwa nunge. Wachezaji wanaume 16 na wanawake 16, wametengwa katika makundi manne ya wachezaji wanne wanne huku wachezaji wawili wa mwanzo wakifuzu kwa awamu ya mwondoano. Mashindano hayo yatakamilika kesho.