Vyuo Zaidi Vya Mafunzo Ya Matibabu KMTC Kuanzishwa

Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha mafunzo ya matibabu nchini KMTC Profesa Philip Kaloki amesema kuwa serikali ina mipango ya kujenga angalau chuo kimoja zaidi cha mafunzo ya matibabu katika kila kaunti kote nchini. Profesa Kaloki alisema kuwa vyuo hivyo vitatoa mafunzo ya kitaalamu zaidi ili kutoa huduma bora kwa wananchi . Profesa kaloki aliyekuwa akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa chuo cha mafunzo ya matibabu cha Rachuonyo mjini Oyugis, alisema kuwa vyuo hivyo hufunza asilimia 85 ya wahudumu wote wa afya kote nchini . Kaloki aliwashukuru viongozi wa kaunti ya Homa Bay County na serikali ya kitaifa kwa ushirikiano wao bora uliowezesha kujengwa kwa vyuo hivyo.