Vyuo Vikuu Vyaathirika Kufuatia Marufuku Ya GMO

Marufuku iliyowekwa na serikali kuhusu mazao yaliyobadilishwa maumbile GMO imeathiri vyuo vikuu kwa kiwango kikubwa.

Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamekutana mjini Nairobi wakiitaka serikali isitishe marufuku hiyo ambayo imesababisha wanafunzi wengi kukosa kazi.

Wanafunzi hao wakiongozwa na kiongozi wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Nairobi Babu Owino wamesema maelfu ya wanafunzi wanaosomea somo la teknolojia ya kilimo wamekosa kazi na wanataka bunge ishinikize shirika la mazingira nchini NEMA kuanza kutoa leseni za kufanyia majaribio teknolojia hiyo.