Vyuo Vikuu Viwili Kupewa Jukumu La Mfumo Wa Elimu Wa Digitali

Kundi linaloongozwa na chuo kikuu cha Moi na lingine likiongozwa na chuo kikuu chaA� kiufundi cha Jomo Kenyatta yamechaguliwa kuwasilisha mapendekezo yao ya kueneza mfumo wa elimu wa dijitali katika shule 150 nchini.Mpango huo unajumuisha kusambazwa kwa vipatakilishi katika zaidi ya shule elf 22 za umma nchini.Halmashauri ya teknolojia ya habari nchini imesema kundi linaloongozwa na chuo kikuu cha MOI na shirika la JP SA Couto litatekeleza mpango huo katika kaunti 26 ilhali lile linaoongozwa na chuo kikuu cha kiufundi cha Jomo Kenyatta A�na shirika la Positivo BGH likitekeleza mpango huo katika kaunti 21.Makundi hayo mawili sasa yanahitajika kuwasilisha mapendekezo yao katika shule teule 150 kwenye kaunti zote,ambayo yatatathminiwa baadaye kubaini iwapo makundi hayo yanaweza kutekeleza kikamilifu mpango huo wa kusambaza vipatakilishi katika shule zote za umma nchini.