Vyuo Vikuu Vinavyokiuka Sheria Kufungwa

Serikali itavifunga vyuo vikuu vinavyokiuka sheria na kanuni za mwongozo wa kuwa na elimu bora ya vyuo vikuu humu nchini. Waziri wa Elimu Dr. Fred Matianga��i amesema serikali pia itafutilia mbali vyeti vya shahada za digrii ilizowapa wanafunzi wake bila idhini ya Tume ya elimu ya vyuo vikuu kama inavyohitajika kuambatana na hati ya uidhinisho ya kuanzishwa kwa vyuo kama hivyo. Akiongea baada ya kutoa barua ya uidhinisho wa muda kwa chuo kikuu cha kimataifa cha RAF katika jumba la Jogoo Dr. Matianga��i alielezea wasi wasi kwamba baadhi ya vyuo vikuu vinawachukua wanafunzi kwa masomo ya shahada za digrii bila kutimiza mahitaji ya kimsingi.