Vyama Vyatekeleza Kampeni Za Dakika Ya Mwisho Malindi

Zikiwa zimesalia chini ya siku nne kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mdogo katika eneobunge laA� Malindi, vyama vya kisiasa vinatekeleza kampeni za mwisho mwisho kuwashawishi wapigaji kura. Kundi la kampeni la muungano wa CORD likiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Ondiga liliandaa mikutano katika wadi ya Kakuyuni na wanatarajiwa kuandaa mkutano mkubwa leo mjuini Malindi. Mwaniaji wa chama cha JAP akiongozwa na mbunge wa Kilifi kaskazini Gideon Munga��aro walipeleka kampeni zao za nyumba hadi nyumba kwenye wadi ya Jilore kuwashawishi wapigaji kura. Naibu rais William Ruto leo atajiunga na kundi la kampeni la jubilee ili kuimarisha kampeni zao. Akihutubu kwenye mkutano huko Kakuyuni, Odinga aliishtumu serikali kwa kushindwa kutimiza ahadi ilizotoa wakati wa kampeni akisema kwamba muungano wa CORD uko tayari kutwaa hatamu za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao.