Viwavi wasababisha uharibifu mkubwa kwa mimea kaunti ya Migori

Wakulima wa Mahindi kwenye Kata ya Kakrao, Kaunti ya Migori, wameingiwa na wasi wasi baada ya mashamba yao kuvamiwa na viwavi. Wadudu hao wameharibu mashamba kadhaa ya mahindi huku kukiwa na hofu kwamba huenda wakavamia mimea mingine. Kulingana na mkulima mmoja Pius Amara, wengi wa wakulima sasa wanafikia kunga��oa mimea yao kama njia moja ya kukabiliana na wadudu hao waharibifu. Aliongeza kwamba juhudi za kupata usaidizi kutoka kwa maafisa wa kilimo katika ngazi za kaunti hazihafua dafu.

Wadudu hao ambao wanafahamika kwa kusababisha uharibifu mkubwa, wamevamia piaA� mashamba katika baadhi ya maeneo ya Rongo, Awendo naA� Uriri kwenye kaunti ya Migori. Wakati huo huo; Visa vya uvamizi wa viwavi vimeripotiwa pia katika sehemu mbali mbali za Jamhuri, ikiwa ni pamoja na kaunti za Trans-Nzoia, Nakuru, Kakamega, Nandi, Busia, Bungoma, Uasin Gishu, Taita Taveta na Kwale, huku wadudu hao wakishambulia hasa mahindi.