Vita na magonjwa yasababisha idadi kubwa ya watoto wanaofariki kila siku

Shirika moja la kimataifa la kutoa misaada linakadiria kuwa takriban watoto 130 au zaidi hufariki dunia kila siku kutokana na A�nja na magonjwa katika nchi ya Yemen ,ambayo inakumbwa na vita. Kulingana na shirika la Save the Children,mapigano ambayo yanaendelea nchini humo yakiongozwa na muungano wa wanajeshi unaoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa kishia kwa upande wa pili ,huenda yakaongeza idadi ya watoto na watu wazima watakaoangamia A�nchini humo.Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo zaidi ya watoto 50,000 wanadhaniwa wameangamia nchini Yemen kutokana na vita tangu mwaka huu wa 2017. Saudi Arabia ilifunga bandari za nchi hiyo baada ya kombora lililorushwa na waasi kuanguka karibu na mji wake mkuu,Riyadh.Hata hivyo imesema itasitisha harakati hizo baada ya shutuma A�kali za kimataifa na za kutoka ndani. Jana shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya afya-WHO,lile linaoshughukia watoto-UNICEF na shirika la chakula duniani-FAO ,yametoa mwito wa pamoja wakutaka Saudia Arabia kusitisha harakati zake nchini Yemen.