Viongozi Wanawake Kote Nchini Wawataka Vinara Wa Mrengo Wa CORD Kusitisha Maandamano

Viongozi wanawake kote nchini wamewataka vinara wa mrengo wa CORD wasitishe maandamano yao ya kila wiki kutoa fursa ya mashauriano. Kupitia kundi la Warembo na Uhuruto, wanawake hao wanataka upinzani uzingatie katiba katika kushinikiza marekebisho kwenye tume huru ya uchaguzi na mipaka- IEBC. Kulingana na mwasisi wa kundi hilo, Wambui Nyutu, upinzani unapaswa kuwaruhusu viongozi kujadili swala la IEBC bila kuweka masharti na vitisho vya maandamano. Bi Nyutu alisema maandamano hayo yameathiri watu wengi hapa nchini hasa vijana.A�Mrengo wa CORD umesisitisha maandamano yake kote nchini kutoa fursa ya kuanza kwa mashauriano.