Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kuwasilisha rufaa yao

Viongozi wa wanafunzi kwenye vyuo vikuu vya Umma waliwasilisha rufaa yao kwa bunge leo alasiri kutaka lifanye uchunguzi na kukomesha ukatili wa polisi kwenye taasisi za elimu ya juu nchini. Viongozi hao wa wanafunzi ambao walikutana kwenye bewa la Nairobi la chuo kikuu cha Moi kabla kuelekea katika majengo ya Bunge, walimshtumu Inspekta Generali wa polisi Joseph Boinnet na pia waziri wa elimu Amina Mohammed kwa kutofanya lolote kuhusiana na mauaji ya kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Meru Evans Njoroge. Walitaka hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa ambao watahusishwa na ukatili kwenye vyuo vikuu nchini wakati wa migomo ya wanafunzi.