Viongozi wa rift valley washinikiza mandago akamatwe kwa matamshi ya uchochezi

Baadhi ya viongozi wa eneo la Rift Valley wanashinikiza kukamatwa kwaA� gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago na wabunge wawili wa eneo hilo kwa madai ya uchochezi na kutoa matamshi ya chuki. Wakiongozwa na mwenyekiti a baraza la wazee wa jamii Gilbert Kabage, viongozi hao wamehimiza tume ya uwiano na mshikamano wa kitaifa kuwachukulia hatua wanasiasa hao. Kabage anawalaumu Mandago na wabunge Oscar Sudi wa Kapseret na mwenzake wa Nandi Hills, Alfred Keter kwa kuzua uhasama miongoni mwa jamii zinazoishi katika kaunti ya Uasin Gishu. Katibu wa baraza hilo Peter Charagu pia alihimiza tume huru ya uchaguzi na mipaka kuwachukulia hatua za kinidhamu wawaniaji wanaokiuka sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wa vuguvugu la Peoplea��s Power Watch, Jesse Karanja aliunga mkono wito wa kukamatwa kwa wanasiasa hao akisema ipo haja ya kuwachukulia hatua wanasiasa wanaozua uhasama kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti. Eneo la North Rift ni miongoni mwa maeneo yaliyokumbwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu elfu moja walipoteza maisha yao na wengine wengi kufurushwa makwao.